Wakulima wa zao la Pareto Kata ya Ilembo Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya wamelalamika kutokuwa na imani na bei wanayopewa na wanunuzi kama inaendana na ubora wa zao hili kutokana na kukosa mtaalamu wa kuhakiki ubora wa pareto inapofikishwa kiwandani.
Akitoa malalamiko hayo leo tarehe 5 Machi, 2019 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwenye mkutano wa hadhara, Diwani wa kata hiyo Mhe Bunge Njawala amesema kuwa changamoto hiyo inawafanya wakulima kukata tamaa na kilimo hicho cha pareto.
Bw. Njawala amesema kuwa wanunuzi wanachukua pareto ya wakulima kwaajili ya kwenda kupima kiwango cha sumu na hakuna mkulima anayekwenda kuthibitisha katika viwanda hivyo kufanya malipo ya pili ya fedha zao kutozipata.
Aidha, Bw. Njawala amelalamikia pia kuwepo kwa mnunuzi mmoja wa zao hilo na kupelekea kukosa ushindani na kukupaliana na bei yoyote itakayopangiwa na mnunuzi huyo ambae ni Kiwanda cha Pareto Mafinga.
Akijibu malalamiko hayo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila amesema amepanga kuwaita na kuzungumza na wanunuzi wa zao hilo ikiwezekana waanze kuifanyia marekebisho mikataba ya ununuzi ili uweze kumnufaisha Mkulima
“ Haiwezekani Mkoa wa Mbeya ukawa wa pili kwa uzalishaji wa pareto iliyo bora kwa ukanda huu duniani lakini wakulima wasinufaike na kilimo hicho, nitalisimamia kuhakikisha pande zote mbili zinanufaika” Mhe. Chalamila
Naye Hamadi Mbeyale amelalamikia ukosefu wa fedha kwa muda mrefu kwenye vituo vya kuuzia pareto kinyume na kanuni za bodi ya pareto na kuhisi kama bodi hiyo sio msaada kwao kwa kuonyesha upendeleo kwa kiwanda cha pareto
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa