Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Leo amefanya ziara wilayani Mbarali kwa lengo la kukagua mashamba ya mpunga ktk Bonde la Usangu, Viwanda vya Kuchakata Mpunga na kisha kufanya Mkutano wa Hadhara Kata ya Ubaruku.
Amesema kuwa Ili kulinda ekolojia ya Hifadhi ya Mto Ruah ameagiza kilimo kizingatie sheria ya hifadhi ya vyanzo vya Maji ya mita sitini, kubomoa matuta yote yanayokinga Maji kutokwenda mtoni na kutoingiza au kuondosha mifugo yote ktk hifadhi.
Hata hivyo Wananchi kwa pamoja wamepokea maelekezo hayo na wameomba serikali iainishe haraka eneo la mita sitini na wako tayari kupanda miti
Aidha, Mkuu wa Mkoa amepongeza Halmashauri kwa uwingi wa viwanda vya kuchakata mpunga ambapo Kata ya Ubaruku ina viwanda vya kisasa zaidi ya 25 vinavyotoa ajira ya zaidi watu 1200
Amewataka wenye viwanda kuboresha bidhaa YA mchele kwa kuweka nembo na vifungaishio vizuri ili kuhimili ushindani ktk soko na pia kuitangaza mbarali na Mkoa wa Mbeya
Ameeleza Mkoa wa Mbeya una ziada YA chakula tani milioni 3
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa