Mkoa wa Mbeya ameagiza Wakuu wa Wilaya wote kutumia msimu huu wa mvua kusimamia na kushirikiana na wananchi kuendeleza kampeni muhimu ya upandaji wa miti kitaifa ili kuweza kupunguza uharibifu unaosababishwa na ukataji miti na kutunza vyanzo vya maji na kuweza kufikia lengo tuliloweka la kupanda miti 1.5 milioni au zaidi kwa kila Halmashauri.
Mhe Makalla ameyasema hayo katika uzinduzi wa Kampeni za upandaji miti Kitaifa Mkoa wa Mbeya ambapo kampeni hii hufanyika ili kuruhusu wananchi wote wa maeneo husika kushiriki kikamilifu katika kupanda miti kwenye maeneo yao ya makazi.
“ Ni imani yangu kuwa, wakazi wa Vijiji na Mitaa inayozunguka hifadhi hii mtahakikisha kuwa miti iliyopo na inayopandwa kwenye hifadhi hii na pembezoni mwa barabara inatunzwa kikamilifu ili kuboresha hali ya mazingira na uhifadhi wa misitu na vyanzo vya maji katika maeneo yetu”. Mhe. Makalla
Pia Mhe. Makalla amewataka Viongozi wa Siasa na Serikali kudhibiti ufugaji ndani ya hifadhi na kuhakikisha kwamba mifugo yote inafungwa na kuhudumiwa katika maeneo yaliyoruhusiwa pasipo kusababisha uharibifu wa rasilimali za mazingira
Mwakilishi wa Mamlaka ya Mji Bw. Venance Hawela amesema ili kutekeleza kikamilifu jukumu hili mwaka huu mradi wa uhifadhi mazingira Mlima Mbeya umeweka malengo ya upandaji miti 102,000 kwa ajili ya vyanzo vya maji, mapambo na Matunda na kimvuli.
Bw. Hawela amesema kuwa lengo kuu ni kuhamasisha wananchi kuwa na utamaduni wa kupanda miti katika maeneo yao ili kuepusha nchi kuwa jangwa kutokana na kukosekana kwa rasilimali ya misitu.
Aidha amehimiza shughuli za upandaji miti kuendelea na kusimamia shughuli za upandaji miti ziwe ni utamaduni wananchi kupanda miti kwenye maeneo yao na vyanzo vya maji kwani ni muhimu sana kwa maisha ya kila siku.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa