Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mbeya Mhe Amos Makalla ameweka kikaangoni Wakuu wa Wilaya baada ya kuwaagiza kuandika barua za kujieleza kwa kushindwa kutekeleza agizo la Serikali la kufikia asilimia 100 ya uwekaji alama mifugo na kwamba wasipende kumjaribu katika utendaji wa kazi.
Makalla ametoa agizo hilo alipokutana na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wenyeviti wa Halmashauri katika ukumbi wa mikutano akisisitizi kuwa agizo hilo ni la Wizara ya Kilimo na Mifugo katika kufuatilia utekelezaji wa zoezi hilo.
Mhe. Makalla amesema kuwa ifikapo Februari Mosi barua hizo ziwe zimewasilishwa ofisini kwake ili ziweze kuambatanishwa na utekelezaji wa zoezi la uwekaji wa alama mifugo na kuwasilisha wizarani haraka iwezekanavyo.
Aidha, amewatahadharisha Wakuu wa Wilaya kutowahusisha Wakurugenzi wa Halmashauri kuhusu kukwamisha zoezi hilo kwa kuwa jukumu hilo walikabidhiwa wao ili kufikikia malengo waliyopewa na Serikali.
“ Ninawaomba katika hizo barua msiwatwishe mizigo Wakurugenzi kuwa ndio kikwazo, Mimi nilizindua zoezi la uwekaji alama mifugo kila Wilaya toka Mwaka Jana lakini Wakuu wa Wilaya mmelipuuza" Mhe Makalla.
Alisema kuwa Wakuu wa Wilaya wasipende kumjaribu katika utendaji wa kazi na kwamba kila mtu ana wajibu wa kulinda kibarua chake na ufike wakati wa kufanya kazi kwa kujituma na si mazoea kwa Serikali hii ya Awamu ya Tano.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa Mama Mariam Mtunguja amesema kuwa Watendaji wa Serikali wanapaswa kutambua majukumu yao na maagizo kutoka ngazi za juu na kwamba usifike wakati wa kukumbushwa majukumu yao na kuwataka kila Mtendaji atimize Wajibu wake.
Mama Mtunguja amesema kuwa wanapaswa kumtumia vizuri Mkuu wa Mkoa katika uwajibikaji na utekelezaji wa majukumu kwa kuwa anatoa ushirikiano mkubwa na si kumlazimisha kufanya maamuzi magumu.
Aidha amefafanua kuwa katika Halmashauri zote Mbeya Jiji imefanya vizuri kwa kufikia asilimia 100 wakati Mbarali ina 83, Kyela 82, Mbeya DC 81, Busokelo 75 na Rungwe kushika nafasi mwisho kwa asilimia 27 wakati ndio inayozalisha maziwa kwa wingi kutoka Mkoa wa Mbeya
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa