Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amewaagiza wananchi wa Mkoa wa Mbeya ambao wamevamia hifadhi na mapori ya akiba kuondoka kwa hiari katika maeneo hayo kama walivyokubaliana kabla Serikali haijachukua hatua za kuwaondoa ili kulinda uharibifu wa mazingira.
Akizungumza kwenye kwenye kikao maalum cha baraza la Madiwani Chunya Mhe Makalla amewataka wananchi wote waliovamia hifadhi, mapori na vyanzo vya maji wahame kwa hiari ndani ya kipindi cha wiki tatu (3) kabla Serikali ya Mkoa haijaanza kampeni ya kuwaondoa katika maeneo hayo
“Natoa agizo kwa Kamati za Ulinzi na Usalama Kila Wilaya kukagua utekelezaji wa agizo hili kuanzia Septemba 20, 2017 na kwa wale ambao watakaidi agizo hili hatua stahiki zitachukuliwa kwani wananchi walivamia maeneo hayo wamekaidi kuhama kwa muda mrefu na niliamua kuwapa nafasi zaidi pasipo kutii agizo hilo na wananchi hao waliovamia hifadhi wasajiliwe katika vijiji vilivyopo katika vijiji vingine .” Mhe. Makalla
Mhe Makalla amesema kutakuwa na operasheni za kushtukiza katika hifadhi na mapori yote ya akiba kila mara ili kuangalia kama kuna shughuli zozote za kibinadamu zinazoendelea katika maeneo hayo. Lengo kubwa ni kulinda vyanzo vya maji na uhifadhi wa mazingira.
Aidha, Amesema kuwa Katika hatua nyingine Mhe Makalla amewataka wananchi kuendelea kupanda miti kwa wingi ili kuepuka hali ya Ukame ambao utapelekea kuwepo kwa Jangwa katika maeneo yao na kuwa na utamaduni wa kupanda miti ya vivuli na matunda katika makazi na vyanzo vya maji.
Mhe Makalla amewataka Wakuu wa Wilaya zote kukaa na uongozi wa Vijiji vyote vilivyopo katika safu za milima na kuangalia jinsi gani watazuia tabia ya baadhi ya wananchi kuchoma misitu hovyo na kuharibu mazingira.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa