Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera ameamuru Jeshi la Polisi kuwatafuta na kuwakamata Wanachama 17 wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) mkoani Mbeya wakituhumiwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh188 milioni.
Wanadaiwa kuchukua dawa nyingi kwenye vituo vya afya na kuziuza kwenye hospitali binafsi na maduka ya dawa.
Hayo yameelezwa leo Jumanne Julai 6, 2021 na mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera katika mkutano wake na waandishi wa habari baada kupokea taarifa ya ripoti ya upotevu wa fedha kutoka kwa naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel.
Amesema mbali na wanachama hao kushikiliwa na polisi, pia vituo saba vya afya vimebainika kufanyika wizi wa dawa za Sh1.6 bilioni na kwamba uongozi wa mkoa huo kwa kushirikiana na wizara ya afya wametoa muda wahusika kurejesha fedha hizo.
"Ripoti inaeleza wizi umetokana na utoaji wa dawa kwa wanachama waliokuwa wakienda kupata huduma na kupewa dawa kwa wingi na kisha kwenda kuuza,” amesema Homera akibainisha wengi walidanganya kuugua kisukari na shinikizo la damu na kwenda kuziuza hospitali binafsi na maduka ya dawa.
Amesema watafanya uchunguzi na wote waliohusika watasakwa popote walipo na kukamatwa.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa