Mkuu wa wa Wilaya ya Rungwe Mhe Julius Chalya amewataka wananchi wa Mkoa wa Mbeya kutunza mazingira kwani ustawi wa viwanda unategemea mazingira bora ili kuhakikisha usalama na uwezo wa kupata malighafi.
Mhe Chalya ametoa kauli hiyo Juni 5, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwenye kilele cha maaadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambapo kimkoa yamefanyika Kijiji cha Bulyaga Wilaya ya Rungwe.
Mhe. Chalya amesema mazingira na viwanda vinategemeana katika ustawi wake na ukihifadhi mazingira viwanda vinakuwa endelevu kwani viwanda vinategemea malighafi zinazopatikana kwenye mazingira.
Aidha, Chalya amesema viwanda na mazingira vina uhusiano mkubwa na kila kimoja kikitumiwa vibaya kinaweza kumuathiri mwenzake. Hivyo ametoa rai kwa wananchi wote kutunza na kulinda mazingira ili kufaidi matunda ya viwanda, na wawekezaji wa viwanda kufanya uchunguzi wa athari za kimazingira kabla ya kuanzisha viwanda vyao.
Kilele cha maazimisho ya siku ya mazingira duniani uazimishwa kila mwaka ifikapo Juni 5. Kwa mwaka huu kidunia siku hii imeazimishwa nchini India ambapo kauli mbiu ya kidunia inayosema “Pinga uchafuzi wa mazingira unaotokana na bidhaa za plastiki” Kitaifa maazimisho yamefanyika jijini Dar es salaam kwa kauli mbiu inayosema “Mkaa ni gharama; Tumia nishati mbadala”
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa