Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera Leo tarehe 14/08/2021 ametembelea na kukagua Miradi itakayotembelewa na Mwenge Maalumu wa Uhuru mwaka 2021 Wilaya ya Mbarali siku ya tarehe 11/09/2021 katika eneo la Igawa kata ya Lugelele ukitokea Mkoa wa Njombe.
Katika ziara hiyo Mhe. Homera amefurahishwa na miradi iliyopendekezwa na uongozi wa Wilaya ya Mbarali kwa ajili ya kutembelewa na Mbio za Mwenge Maalumu wa Uhuru kwani miradi hiyo imefuata vigezo vya Mbio za Mwenge.
“Niwapongeze kwa kuzingatia vigezo vya Mwenge, Miradi yote ya Mbarali ipo vizuri, kikubwa ni kujipanga vizuri kuupokea hasa kwenye kuhamasisha wananchi, vikundi vya burudani na ngoma za asili.”
“Nawasihi wananchi mjitokeze kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru, kila mwananchi auchukulie Mwenge huu kama wake, wasiwaachie viongozi wa Serikali pekee, mwenge ni wetu sote.” Alisema Mhe. Homera
Miradi iliyotembelewa na Mhe. Homera ni pamoja na eneo la Mapokezi la Mwenge Maalumu wa Uhuru eneo la Igawa, Kituo cha Mafuta cha Nyamuhanga eneo la Igawa, kiwanda cha Kuchakata Mpunga cha Highland Estate eneo la Igawa, Mradi wa Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi shule ya Msingi Igomero, Mradi wa uhifadhi wa Mazingira katika shule ya Sekondari ya Ihanga Mbarali.
Mingine ni mradi wa TEHAMA katika kituo cha afya Mapogoro, mradi wa kikundi cha vijana Bodaboda Mbuyuni, mradi wa huduma ya elimu kuhusu VVU/UKIMWI na Maralia hospitali ya Chimala Misheni, mradi wa utoaji wa huduma ya Lishe kwa jamii ofisi ya kijiji cha Chimala pamoja na eneo la Mkesha wa Mwenge wa Uhuru shule ya msingi Majenje
Kauli mbiu ya Mwenge Maalumu wa Uhuru mwaka 2021 ni “TEHAMA ni Msingi wa Taifa Endelevu, Itumike kwa Usahihi na Uwajibikaji”
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa