Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amewaagiza waratibu elimu kata mkoani Mbeya kuhakikisha wanafanya kazi yao kwa vitendo na ikiwezekana waingie madarasani kukagua wakati walimu wanaendele kufundisha.
Mhe Makalla ametoa agizo hilo kwenye maadhimisho ya kilele cha Wiki la Elimu yaliyofanyika kimkoa jijini hapa na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta hiyo wakiwemo waratibu wa Elimu Kata.
Makalla amesema waratibu wa sasa wameondoka katika misingi rasmi ya kazi yao kwakuwa wanatumia muda mwingi kufanya shughuli zao binafsi badala ya ile waliyopewa na serikali.
Amesema wapo baadhi yao ambao wanadiriki kufanya biashara wakati wa kazi ikiwemo usafirishaji wa abiria kupitia pikipiki maarufu kama bodaboda kwa kutumia kisingizio cha kuwa katika kijiji kingine akiratibu pale wageni wanapomuulizia bada ya kumkoa ofisini.
Makalla pia amesisitiza wakuu wa wilaya na wakurugezni watendaji wa Halmashauri kuweka mkazo katika kuwashirikisha wadau mbalimbali pasipo kujali ukubwa au udogo wa mchango wao kwenye sekta ya elimu hata kama mtu anachangia mfuko mmoja wa saruji.
Amesema ushirikishwaji wa wadau ni jambo muhimu kwakuwa utawezesha kila mmoja kuona yuko sehemu ya mafanikio pale yanapopatikana na pia atajiona ni sehemu ya kufanya vibaya pale yanapopatikana matokeo yasiyoridhisha.
Awali akitoa taarifa ya Elimu ya mkoa, Kaimu Afisa Elimu wa Mkoa wa Mbeya,Gerald Kifyasi amesema miongoni mwa changamoto zinazoikabili sekta hiyo ni pamoja na Ufuatiliaji hafifu wa ufundishaji,wanafunzi kutokula chakula cha mchana mashuleni na uhaba wa miundombinu muhimu mashuleni ikiwemo vyoo na vyumba vya madarasa
Katika maadhimisho hayo pia zawadi mbalimbali za fedha taslimu,ngao na vyeti vilitolewa kwa Halmashauri na Halmashauri zilizofanya vizuri katika sekta ya Elimu sambamba na walimu na wanafunzi waliofanya vizuri.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa