Serikali Mkoa wa Mbeya imesema Mtanzania yeyote anayetaka kusafiri kwenda nchi ya Malawi anapaswa kutambua kuwa atakaporejea atalazimika kuwekwa karantini kwa muda wa siku 14 kwa gharama zake mwenyewe.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila ameyasema hayo mapema leo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Njisi wanaoishi mpakani mwa Tanzania na Malawi na kuwataka wapunguze safari ambazo sio za lazima katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19.
Amesema kuwa wakati huu serikali ikiwa katika mapambano ya kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona ni muhimu wananchi kupunguza safari zisizo za lazima, kuepuka misongamano, kuvaa barakoa na kunawa mikono kwa maji tiririka.
”Mmeusikia ugonjwa ambao kwa sasa unatikisa dunia, ukienda nchi kama Italia, Uhispania na Marekani wenzetu wakifa wachache Sana kwa siku ni 800 kwa hiyo ni vizuri tukaanza kuchukua hatua mapema Sana ili tusifikie huko”. Alisema Chalamila.
Mhe Chalamila amesema kuwa mpaka wetu huu wa Kasumulu unaotenganisha Tanzania na Malawi hautafungwa lakini agizo la kwanza Mtanzania yoyote atakayetoka kwenda Malawi aende ila atakaporudi atatengwa karantini kwa muda wa siku 14 kwa gharama zake mwenyewe.
Aidha Mkuu wa Mkoa amesema Serikali imeona hakuna ulazima kwa madereva wanaosafirisha magari yanayokwenda nje ya nchi (IT) kuwa na abiria zaidi ya mmoja kwenye magari hayo
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa