Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Comrade Juma Homera amewataka Wataalamu na Maafisa Manunuzi Kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya kuwa na Nidhamu ya Matumizi ya Fedha za Umma na kujiepusha na Udanganyifu wa aina yeyote hasa wawapo katika Utekelezaji wa majukumu Yao ya Kazi.
RC Homera ameyasema hayo leo wakati akifungua Kikao Cha Chanjo ya Polio kwa awamu ya pili ambapo mbali na Agizo hilo ameipongeza Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa kwa Uratibu Mzuri wa Shughuli za Chanjo hasa awamu ya kwanza hata katika shughuli zingine za Afya.
"Nichukie Nafasi hii kumpongeza RMO na Timu yake maana Baada ya Uzinduzi wa awamu ya kwanza kule Iyela malengo ilikuwa kuchanja Laki 5- Laki 6 lakini tulivhanja Watoto zaidi ya Laki Saba sawa na asilimia 124.82 kwahyo tulivuka malengo Kwakweli tujipigie Makofi"
Aidha RC Homera ameiagiza Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa kusimamia Kikamilifu Fedha zinazoletwa na Serikali na kudai anataka kuona Matokeo zaidi tena Matokeo Chanya hasa katika Fedha zilizotengwa kwaajiri ya Usafi na Mazingira(OSHA).
Viongozi wa Dini na wa Kimila wakapata Nafasi ya Kutoa maoni Yao katika kikao hicho ambapo Yako Mengi wameishauri Serikali ya Mkoa wa Mbeya kuyaboresha ili kuendelea kuisaidia Jamii inayowazunguka.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa