Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Dr. Festo Dugange amewatakaMganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kiwanja Mpaka kuhakikisha wanaongeza kasi yaukusanyaji wa mapato na kuanza kufanya ukarabati wa jingo la kituo hicho.
Dr. Festo amesema hayo wakati wa ugawaji wa vifaa tibavilivyotolewa na Shirika la WRP-T Kwa Mikoa ya Mbeya, Songwe,Rukwa na Katavimapema tarehe 13.2.2021 kwenye viwanja vya Kituo cha Afya Kiwanja.
Dr. Dugange amesema ili Kuboresha huduma vituo vya Afya ni lazimavidhibiti ukusanyajo wa mapato yake ili yaweze kutumika kwenye uendeshaji wakituo na sio kusubiria fedha kutoka Serikali kuu.
“Nimeanza kwa kikagua kituo hiki cha Kiwanja Mpaka nimeambiwakuwa makusanyo kwa siku ni shilingi laki tatu ilihali watu wanaotibiwa kwa sikuhapa ni mia tatu kwa hesabu za haraka hataka kituo kinatakiwa kukusanya sichini ya shilingi laki sita kwa siku.
Amesema kuwa bila kutumia akili nyingi utagundua tu kuwa hapamapato yanavuja na nyie mko tu hamna wasiwasi kabisa hatuwezi kwenda hivyo nilazimaMianya hii ya upotevu wa mapato idhibitiwe ipasavyo na mapato yaonekane”alisema.
Aliongeza kuwa “Kituo hiki kiko katikati ya Mji kinatakiwa kiwena hadhi lakini muonekano wake hauvutii Kituo kimechakaa sana majengo chakavuhata rangi mnashindwa kupiga au kufanya ukarabati mdogo mdogo” alihoji Dr.Dugange.
Aliwataka watalaam wa Afya Jijini Mbeya kujitathmini na kuwekamikakati itakayoleta tija katika utoaji wa huduma bora za Afya Jijini humo. Katikakutekeleza maagizo hayo alitoa muda wa miezi miwili kwa wataalam hao wa Afyakuhakikisha kuwa mifumo ya ukusanyaji wa mapato kwenye vituo vyote Jijini Mbeyaunaimarishwa na kuahidi kurudi Mwezi Mei 2021 kukagua utekelezaji wa maagizohayo.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa