Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera leo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rungwe kuwachukulia hatua Watendaji 18 wanaotuhumiwa kusababisha upotevu wa zaidi ya sh milioni 70 za mapato ya Halmashauri.
Mhe Homera ameyasema hayo mapema tarehe 14.6.2021 amekutana na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ambapo ameagiza watendaji hao kurudisha fedha hizo ndani ya siku saba kabla vyombo vya sheria havijawachukulia hatua
“Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wakuu wa idara kuomba fedha ambayo haijawekwa kwenye akaunti za halmashauri (fedha mbichi) kwa visingizo vya ziara za viongozi, sasa sisi tutakuchukulia hatua wewe mtendaji unayetoa fedha hizo” RC Jomera
Aidha ameipongeza Halmashauri Kwa kukusanya MAPATO Kwa ufanisi mkubwa hadi kufikia asilimia 93% hali itakayochochea Maendeleo Kwa mwananchi mmojammoja na taifa Kwa ujumla .
" Menejimenti na watumishi wote mmefanya kazi kubwa ya kukusanya mapato, hongera Sana! Niwaagize sasa watendaji wa kata kuleta marejesho Kwa wakati kwa kuwa hizi ni fedha za umma"
"Naamini asilimia Saba iliyobaki inaweza kumalizika haraka iwapo ukusanyaji wa MAPATO ukifanyika Kwa bidii Kwa siku chache zilizobaki kufunga mwaka huu wa fedha"
Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Bi. Angelina Lutambi (Kwenye skafu katikakati) ameomba watumishi wote kutoa huduma bora Kwa wananchi, kuzingatia uadilifu kazini, kutenda haki ikiwa ni pamoja na kujenga mahusiano mazuri kazini.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe. Julius Chalya amesema kuwa watumishi wameendea kufanya kazi Kwa bidii huku miradi kadhaa ikitekelezwa akiutaja mradi mkubwa kupanua Chanzo cha maji Ikama ( MTO Mbaka) ambao utaharakisha usambazaji wa maji katika Mji wa Tukuyu ambapo katika hatua za awali jumla ya shilingi Million 500 zinatarajiwa kutumika.
Awali Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bi. Loema Peter amesema kuwa Rungwe ina jumla ya watumishi wenye ajira ya kudumu wapatao 3226 na vibarua 82 na serikali imeendelea kulipa madai ya watumishi mbalimbali pamoja na promosheni ikiwa ni hatua ya kuongeza ari na ufanisi kazini.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa