Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila amewaagiza watumishi wote wa umma waliochukua mikopo katika Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Kiwira kurudisha fedha hizo kabla ya tarehe 1 April, 2019.
Mhe. Chalamila ameyasema hayo leo Kata ya Kiwira wilayani Rungwe alipokuwa akiongea na wanachama wa Kiwira SACCOS pamoja na bodi na watendaji wa chama hicho.
Mhe. Chalamila amesema kuwa haiwezekani Chama kinatengeneza mazingira mazuri ya kuwanufaisha wanachama wake lakini watumishi watumie elimu zao kuwaibia wanachama hao.
" Leo hii kuna Hakimu hapa anadaiwa karibu milioni 48 na chama, mnajuaje kama hizo kesi zinazofunguliwa na wadaiwa sugu yeye ndo anawaita ili acheleweshe hukumu?" Mhe Chalamila
Aidha, Mhe Mkuu wa Mkoa amewashauri wanachama hao kuangalia namna ya kubadili sheria na kuhakikisha watumishi wa umma makato yao yanaidhinishwa na mwajiri wake ili yakatwe kupitia mshahara yao.
Akisoma taarifa ya ukaguzi maalumu wa Chama hicho Afisa Ushirika wa Wilaya Bw Thadey mwambeso amesema kuwa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Kiwira kimeshindwa kujiendesha na kushindwa kutoa huduma za fedha kwa wakati kwa wateja wake pamoja na wanachama kutokana na kuwa na madeni makubwa na kutosimamia ureshwaji wa mikopo.
Bw. Mwambeso amesema kuwa moja changamoto ni watumishi 14 wa umma kama mbalimbali wakiwemo polisi, watendaji,Hakimu na daktari kutorejesha mikopo yao kwa wakati.
Naye Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoani Mbeya Bi Angela Maganga amesema kuwa bodi imeshindwa kusimamia chama na kukiuka kanuni na taratibu za uendeshaji wa chama ikiwemo kushindwa kuwasimamia watendaji mpaka wanajikopesha fedha na kutolipa fedha hizo kwa riba.Bi Maganga amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya Ushirika namba 6 mwaka 2013 jedwali namba 4 kifungu namba 7 anaivunja bodi ya Kiwira SACCOS kwa kushindwa kusimamia masuala ya chama hicho na kupelekea kushindwa kutoa huduma kwa wanachama na wateja wake.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa