Na Esther Macha,Rungwe
SERIKALI Mkoani Mbeya imewataka watumishi wa umma kutoa taarifa sahihi kwa wananchi za mapato na matumizi ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao kupitia mikutano ya hadhara na mbao za matangazo
Wananchi wakijua namna kodi zao zinavyotumika watapunguza malalamiko na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ambazo zinakuwa zinafanyika katika maeneo yao.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Albert Chalamila wakati kikao cha baraza la madiwani kilichokuwa kikijadili majibu ya hoja na mapendekezo ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG) kwa mwaka 2017/2018 kwa halmashauri za Wilaya ya Busokelo na Rungwe.
Aidha Chalamila aliwataka watumishi wa umma kuhakikisha kuwa wanasimamia fedha za umma na kutumika kwa maslahi ya umma na siyo maslahi ya mtu binafsi.
“Lakini pia ongezeni ukusanyaji wa mapato ya ndani na ni lazima yaendane na nidhamu ya matumizi na jukumu lenu ni kusimamia na kuhakikisha kuwa mapato yote yanayokusanywa kutoka kwenye vyanzo vya ndani na ruzuku ya serikali kuu yanatumika katika malengo yaliyokusudiwa”alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Hata hivyo Chalamila alisema ufuatiliaji wa mara kwa mara ufanyike ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa na manunuzi yote ya umma yanayofanyika yana thamani ya fedha iliyotumika.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kikao hicho pia kilikuwa kinapitia utekelezaji wa mapendekezo ya CAG kwa mwaka 2017/2018 na hoja ya miaka ya nyuma ili kuona mapungufu yaliyobainishwa kwa halmshauri ya Busokelo na jinsi yalivyoshughulikiwa na namna ilivyojipanga kwa kaguzi zijazo.
Akizungumzia kuhusu halmashauri ya wilaya Rungwe kupata hati isiyoridhisha kwa mwaka 2017/2018 Chalamila alisema zilizoanishwa na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali bbadhi ni malipo yenye viambatisho pungufu sh. Mil.114,409,000,hati za malipo ambazo hazikuonekana kwenye ugaguzi sh.mil.8,645,000 pamoja na vitu vingine.
Kwa upande Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya ,Mariamu Mtunguja alisema kati ya wilaya tano za Mko wa mbeya wilaya ya Rungwe pekee ndo wametia doa kwa kupata hati isiyoridhisha kitendo hiki si kizuri kabisa.
“Aidha aliwataka viongozi wa halshauri ya wilaya Rungwe kuwa na ushirikiano kwa wakaguzi wanapofika katika halmashauri zao na kwamba kama wanahitaji taarifa yeyote watoe kusiwepo na tabia ya kuficha taarifa.
Mkuu wa Wilaya Rungwe, Julius Charya alisema kwamba baada ya kufanyika ukaguzi halmashauri ilipata hati yenye mashaka na kuwa hali hiyo ilitokana na usimamizi hafifu kwenye miradi ya maendeleo iliyopita na kwamba ipo haja kwa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri kuchukua hatua kwa watendaji wasiowajibika na madiwani nao wawe wasimamizi wazuri.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa