Watumishi wa Serikali Mkoa wa Mbeya wametakiwa kujitokeza kupima maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kwa lengo la kutambua afya zao na kuishi kwa furaha kuunga mkono agizo la Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kasim Majaliwa alilotoa kwa Wakuu wa Mikoa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Paul Ntinika alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha wananume kupima VVU ili watambue Afya zao katika Viwanja Vya Ruanda Nzovwe Jijijni Mbeya
Mhe. Ntinika amesema kuwa ataanza kwa kuwahamasiha watumishi katika halmashauri za Mbeya na Jiji kwa kuanzia ngazi za kata, vijiji ili Jamii ione mfano na kuhamasika kupima na kufikia Malengo ya Serikali kupunguza maambukizi mapya.
“ Ni lazima Watendaji wa Serikali tuwe wa kwanza kuamasika kupima VVU na si kushinikiza Jamii pekee yake kutambua umuhimu wa upimaji. Kwa hiyo nawataka kutakuwa nyuma katika kufanikisha hili” Alisema
Mhe Ntinika amewaomba viongozi wa dini kutumia nafasi zao katika nyumba za ibada kuwahamasiha wanaume kupima afya zao ili wajitambue na kuishi kwa furaha.
Akisoma taarifa ya Mko kwa niaba ya Katibu Tawala, Katibu Tawala wa Msaidizi Mipango na Uratibu Bw. Conrad Millinga amewataka Vijana kujikita katika shughuli mbalimbali za Kiuchumi na kwamba Serikali iko bega kwa bega katika kuhakikisha kuwawezesha Kiuchumi.
Bw Millinga amesema kuwa amefurahishwa kuona wasichana balee wa kikundi cha Umoja kutoka Kyela walivyojikita katika ujasiriamali wa kufuma mikeka kutengeneza herein, batiki na Mahitaji mengine ya majumba ambapo kunawasaidia kuepuka vishawishi katika mazingira yao.
Mkoa wa Mbeya unashika nafasi ya 3 kitaifa kuwa na maambukizi ya asilimia 9.3 ikilikanisha na asilimia 5 za Serika ambapo bado Mkoa unaendelea kupunguza maambukizi mapya ili kufikia Malengo ya Serikali.
Katibu Tawala wa Mkoa akipima Maambukizi
Msanii Izzo B
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa