Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila amewataka Wawekezaji wenye Asili ya Kichina kufuata sheria na taratibu za nchi hasa katika kusimamia nidhamu ya watumishi wao katika maeneo ya uwekezaji
Mhe Chalamila ameongea hayo leo ofisin kwake alipokutana na wawakilishi na wawekezaji wenye asili ya kichina mkoa wa Mbeya baada ya kupokea malalamiko ya kunyanyaswa kwa baadhi ya watumishi.
“Kikao hiki ni kwa ajili ya kuweka sawa kwani Mkoa Mbeya unawahitaji sana wawekezaji wa kigeni hususani wanaotoka China kuwekeza katika maeneo mbalimbali lakini mnapaswa kusimamia sheria na taratibu za nchi hii”. Mhe Chalamila
Aidha, Chalamila amewahaadi ushirikiano wa kutosha kutoka katika vyombo vya ulinzi na usalama na kuwahakikishia kusaidia kurahisisha taratibu zote za kuwekeza katika kuendeleza na kukuza uwekezaji Mkoa wa Mbeya
Kamanda wa Polisi Mkoa Ulrich Matei amewataka wawekezaji hao kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi pale ambapo wanaona wafanyakazi wao wanapofanya uhalifu wa namna yeyote ili waweze kushughulikiwa kisheia badala ya kujichukulia sheria mkononi
Mshiriki wa Mkutano huo Yung Xinyu alitumia nafasi hiyo kuomba radhi kwa watanzania baada ya baadhi ya wachina kuwashambulia wafanyakazi wao wa kitanzania na kusema watatumia mkutano huu kama sehemu ya kuimarisha mahusiano na biashara zao.
Aidha xinyu ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuwaamini na kuwashirikisha katika baadhi ya miradi ya maendeleo hasa ya barabara katika Mkoa wa Mbeya
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa