Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezindua Mpango Kabambe wa Jiji la Mbeya 2019-2039.
Uzinduzi wa Mpango huo umefanyika leo tarehe 21 Februari 2023 Jijini Mbeya na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.
Akizungungumza wakati wa mpango huo, Dkt Mabula alisema lengo kuu la kuandaa mpango kabambe wa Jiji la Mbeya ni kutoa dira ya namna Jiji la Mbeya litakavyopaswa kukua na kuendelezwa kwa kipindi cha miaka 20 kuanzia 2019-2039.
"Mpango huu unaainisha mikakati ya uendelezaji na uboreshaji maeneo yazamani yaliyojengwa kiholela kama vile sehemu za maeneo ya kata Sinde, Mahanga, Mabatini, Forest ya Zamani Ilomba na Simike na maeneo kongwe yaliyochakaa sana" alisema Dkt Mabula.
Mpango kabambe uliozinduliwa umetaja mikakati minne ya kusimamia ukuaji na maendeleo ya Jiji la Mbeya ambayo ni uendelezaji upya maeneo kongwe, kurasimisha makazi ambayo kimpango miji hayajaathirika sana lakini kuna uwezekano wa kupata miundombinu, kusimamia yasiyo athirika kwa kuvamiwa na ujenzi holela pamoja na mkakati wa kuanzisha miji ya pembezoni.
Dkt Mabula ametoa wito kwa taasisi zinazotoa huduma mbalimbali kwenye Jiji la Mbeya kutumia Mpango kabambe ulioandaliwa katika utekelezaji wa shughuli zao na miradi mbalimbali ya maendeleo.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa