KATIKA kuadhimisha wiki ya maji duniani, Waziri wa Maji naUmwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisiya Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Jiji la Mbeya.
Sambambana hilo Waziri pia alizungumza na wadau wa maji Mkoa wa Mbeya ambapo kwa pamojawalijadili changamoto na jitihada za kuhakikisha rasilimali za Maji zinatunzwa.
Aidha Waziri ameziagiza Mamlaka za Maji nchini kuhakikisha zinalipia huduma yakuchukua maji kwenye mabonde kila mwezi ili kupata fedha za kusaidia utunzajiwa vyanzo vya maji.
Alisema ofisi za Mabonde ya maji zina majukumu makubwa ya kuhakikisha vyanzo vya majivinatunzwa kwa ajili ya manufaa ya vizazi vilivyopo na vizazi vijavyo lakiniyanakabiliwa na changamoto ya fedha hivyo njia pekee ni kupata kutoka kwenyemamlaka zinazochukua maji hayo.
Aidha alitoa wito kwa Mamlaka za Maji kuhakikisha zinadhibiti upotevu wa maji kwakuwa unaingiza hasara kwa serikali kutokana na maji yanayopotea ni majiyaliyotibiwa na kusukumwa kwa umeme.
Alisema kiwango cha kimataifa cha upotevu wa maji hakitakiwi kuzidi asilimia 20 hivyokila Mamlaka kuhakikisha hazizidi kiwango hicho ikiwa ni pamoja na kuondoakabisa.
Awali akisoma taarifa kwa Waziri, Afisa Biashara wa Mamlaka ya Maji na Usafi waMazingira Mbeya, Venance Hawera kwa niaba ya Mkurugenzi alisema Mamlakainamikakati ya kuhifadhi vyanzo vya maji kwa kuwashirikisha wadau kwa kutumiaulinzi shirikishi.
Alisema mikakati mingine ni pamoja na kuongeza idadi ya wateja wa maji safi na majitaka mtandao wa maji uweze kuwafikia wananchi hadi majumbani kwao.
Aliongeza kuwa matarajio ya Mamlaka ni kuongeza chanzo cha maji kutoka Mto Kiwira uliopoWilaya ya Rungwe ambacho kitazalisha Lita Milioni 65 kwa siku ujazo ambaoutaongeza uzalishaji uliopo na kufikia Lita Milioni 115 kwa siku.
Alisema mradi huo wa maji kutoka Mto kiwira kilomita 37 kutoka Mbeya mjini utazalishamaji kwa njia ya mseleleko na kuongeza kiwango cha maji kitakachodumu hadikufikia mwaka 2036 mradi ambao utagharimu shilingi Bilioni 42 hadi kukamilika.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa