Lola ni miongoni mwa vijiji vinavyounda kata ya Upendo tarafa ya kipembawe, Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya, Kijiji hicho kina Kaya 116 zenye wakazi 3735 kati yao wanawake ni 1863.
Licha ya kua na wakazi wengi Kijiji Cha Lola kimekua kikikabiliwa na shida kubwa ya upatikanaji wa huduma za afya na kulazimika kuzifuata umbali wa zaidi ya kilomita 30 kutoka kijijini hapo hadi mamlaka ya mji mdogo wa Makongolosi.
Kutokana na shida hiyo ya kinamama kujifungua njiani wakifuata huduma za uzazi, wakalazimika kujichanga ili kuanza ujenzi wa Zahanati kwenye Kijiji chao mwaka 2021 baada ya kupata zaidi ya millioni 14 Kwa aajili ya ujenzi huo, na baadae kuungwa mkono na serikali, ilipo wapatia millioni 50 mwaka 2023 ili kukamilisha ujenzi.
Hatimae zahanati hiyo imezinduliwa na Mwenge wa Uhuru 2024 na kuwafanya Wananchi kuondokana na Tatizo hilo la kufuta huduma za Afya kwa zaidi ya Kilomita 9 kwenda zahanati ya Upendo na zaidi ya Kilomita 30 kwenda Kituo cha Afya Makongolosi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Godfrey Mnzava Amesema Serikali itaendelea kuboresha Huduma za Afya hivyo amewataka Wahudumu kuwa na Lugha Nzuri kwa Wagonjwa hasa wanapotoa huduma licha ya Kuwataka Wananchi pia kuonesha Ushirikiano kwa Viongozi na Watoa huduma za Afya.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa