Zaidi ya milioni 400 zimepangwa kukamilisha mradi wa ujenzi wa barabara ya Moravian kwa urefu wa km 1 kiwango cha lami ikiwa ni moja ya utekelezaji wa ahadi ya Hayati Dkt John Pombe Magufuli wilayani Chunya.
Akisoma taarifa ya maradi huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya , Mhandisi Mang’ara Magoti amesema kuwa hadi sasa mkandarasi M/S Kagwa General Supplies amekamilisha asilimia 59 na tayari amelipwa zaidi ya shilingi milioni 47
Mhandisi Magoti amesema kuwa kazi zilizofanyika ni pamoja kusafisha eneo, kuchonga barabara, kuweka kifusi cha kitako cha kwanza cha barabara, kuweka kifusi cha pili ambacho kitaweka saruji kwa ajili ya kupata kitako na kujenga kalvati nane
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amemtaka Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini Wilaya ya Chunya kuendelea kufuatilia fedha kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo kwani ni urithi uliochwa kwa Wananchunya na Hayati John Magufuli
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa